SIGN IN TO CHAT

WELCOME TO ALLAMANO SEMINARY - MOROGORO

TO PROCLAIM THE GOSPEL TO ALL NATIONS

Friday, May 24, 2013

ALLAMANO SEMINARI

ALLAMANO SEMINARI
Ni seminari ya shirika la wamisionari wa Consolata ambao wanafanya kazi katika nchi mbalimbali zaidi ya ishirini. Na hapa Tanzania wapo katika majimbo ya Dar-es-saalam, Iringa, Njombe, Morogoro, Singida, na sasa wameanza utume katika jimbo la Dodoma.
Seminari hii ilianzishwa mwaka 1993, na mpaka sasa imetoa mapadre ambao wanafanya kazi katika nchi mbalimbali na waseminari ambao wanaendelea na masomo yao katika nchi mbalimbali wakiwa katika hatua mbalimbali. Hii ni nyumba ya malezi ambapo vijana wenye nia ya kujiunga na shirika wanapata malezi pamoja na kusoma masomo ya Falsafa ambapo kijana anasoma kwa kiwango cha Shahada.
Seminari hupokea vijana kutoka mikoa mbalimbali hapa nchi ambao hujiunga baada ya kumaliza kidato cha sita na kuwa na sifa za kuendelea na chuo kikuu. Kabla ya kuingia katika nyumba hii ya malezi, kijana hutakiwa kuwa na mawasiliano na mkurugenzi wa miito wa shirika kwa kuandika barua ya maombi na ikiwezekana kuonana naye.

Vijana katika nyumba hii huandaliwa kuwa wamisionari ambao kama vile Maria alivyoleta Faraja ya kweli Duniani yaani Yesu Kristu, nao hufinyangwa ili kuwa wahudumu wa kanisa kwa njia ya kueneza injili popote dunia.