SIGN IN TO CHAT

WELCOME TO ALLAMANO SEMINARY - MOROGORO

TO PROCLAIM THE GOSPEL TO ALL NATIONS

KISWAHILI

Ni baada ya Mkutano kuisha wa wakuu wa shirika la Wamisionari wa Consolata Tanzania, ndipo wakuu hao walipoamua kwenda kupata mapumziko mafupi maeneo ya Bagamoyo, Wakuu wengine walikuwa wanapeana michapo mbalimbali na wengine walikuwa wanapata vinywaji ilimradi tu kila Mtu miongoni mwao apate furaha yake. Ndipo Padre Masawe alipoamua kuingia majini na Padre mwenzake kutoka Kongo ili waogelee, kwani hiyo ndiyo burudani yao.

Baada ya kuogelea kwa muda, ndipo Mapadre hao walipoamua kutoka majini ili kurudi nyumbani, ghafla Padre kutoka Kongo alishangaa kutomuona mwenzake, aliamua kurudi nyuma ili kumuangalia, ndipo alipotoka majini na kutoa tarifa kwa wenzake kuhusu kutoonekana kwa Padre mwenzao (Padre Masawe). Baada ya kumtafuta bila mafanikio siku iliyofuata walimkuta amefariki akiwa ufukweni mwa baharí.
Tarifa za kifo cha Padre Masawe (Mkuu wa shirika la Consolata Tanzania) zilianza kuenea baada ya kuthibitika kwa kifo chake, watu mbalimbali walianza kutuma salamu za rambirambi kwa ndugu Wa Consolata popote walipo. Mimi binafsi niliposikia habari za kifo cha Padre Masawe, niliumia sana, nilipatwa na maumivu makali sana ndani ya moyo wangu, furaha yote ya sikukuu ya iddi iliniisha. Ingawa Padre Masawe sikuwahi kumuona kwa sura enzi ya uhai wake.

Kwanini Niliumia Kutokana na KIFO Chake?????????
Niliumia kutokana na sababu zifuatazo: Mosi; Elimu yangu ya kidato cha 5 na 6 niliipata katika shule ya wa Consolata Mafinga Iringa (Consolata Seminary) hivyo basi kwa upande mwingine wa shilingi mimi ni
MCONSOLATA, naamini kwamba miongoni mwa watu waliokuwa wanatuombea wanafunzi wa shule ya Seminary ya Consolata, Padre Masawe naye alikuwa miongoni mwao, hivyo maombezi yake kwa Mama Bikira Maria Consolata (Mfariji) yalinifanya nisome vizuri, niwe na afya njema, na vilevile ni faulu vizuri masomo yangu.
Pili; Niliumia kwa sababu tangu nilipoanza kumsikia Padre Massawe hata kabla ya kuwa Mkuu wa shirika hapa Tanzania, kwanza nilisikia utendaji wake wa kazi ambapo kila kazi aliyopewa na shirika aliifanya kwa weledi na majitoleo makubwa. Hivyo shirika limepoteza tunu kubwa sana.
Tatu; Mawazo yake ya kimapinduzi katika Shirika la wa CONSOLATA yamepotea ghafla.
Nne; Wamisionari wa Consolata sio kwa upande wa Tanzania tu, bali na Dunia kwa ujumla wamepoteza kijana shapu, shupavu na mchapakazi.

Tano; Wamisionari wa Consolata wanajishughulisha na kazi mbalimbali za kijamii, JUA lililozimika ghafla (Padre Masawe), alikuwa na vipindi katika redio Tumaini na alisimamia gazeti la “ENENDENI” la wamisionari wa Consolata Tanzania, hivyo basi, mawazo yake ya kimapinduzi katika jamii ya Tanzania hatutayapata tena. Sababu hizo za msingi ndizo zinazoniumiza sana moyoni mwangu.
Poleni sana Ndugu zangu wapendwa wa Consolata kwani JUA lililozimika ghafla lilikuwa na mawazo ya kimapinduzi, Mpenda Elimu na Muombezi wetu sisi wa Consolata (Mimi sio Mseminari wa Shirika la Consolata, ila ni MCONSOLATA kwa sababu elimu yangu na malezi mazuri nimeyapata seminari ya Consolata – Mafinga Iringa), pia JUA hilo lilikuwa ni muombezi wa Kanisa la Mungu na Dunia kwa ujumla.
“JUA” lililozimika uzidi kutuombea sisi uliotuacha katika dunia hii na sisi pia tunazidi kukuombea ili upumzike kwa Amani.

BWANI ALITOA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIHIMIDIWE AMINA.







   Mama ni mlezi mkuu wa familia. Ni mama ambaye anahusika katika kulea watoto wake pamoja na mumewe kama anaye. Tunamhitaji mama katika maisha yetu. Ni nani asiyetambua umuhimu na upendo wa mama? Achilia mbali kwamba kuna siku aliwahi kukuumiza ukafikia hatua ya kusema huyu si mama yangu. Au alifanya jambo ambalo mpaka sasa ukifiria halikuingia akili mwako, na kama ni kweli mama yako alifanya hivyo, lakini tambua mama ni mama na atabaki kuwa mama yako. Anaudhaifu na mapungufu yake kama binadamu lakini bado anayonguvu ya kusema mwangu, umenisumbua sana katika utoto wako, ujana na hata katika uzee wako bado sikukuache. Tunamtambu mama kwa majukumu mengi aliyanayo hususani mama ni mlezi mkuu wa familia.   
   Mama huyu anakutana na magumu mengi lakini bado hakati tamaa, anajijengea moyo wa uvumilivu hata kama mateso anayoyapata yanakatisha tamaa, lakini anajipa moyo akiamini ipo siku yatakwisha. Inanisikitisha sana kuna baadhi ya akina mama au dada hawapo tayari kupokea majumu ya kulea familia, utasikia wakisema ili kuwa bahati mbaya, sikudhamiria kulea, mimi bado mwanafunzi, haukuwa mpango wangu, alinidanganya nikaamua kufanya hivyo. Tambueni kwa Mungu hakuna bahati mbaya, yote yanapangwa kutendeka wakati utimiapo, kwani hafikiria vile binadamu afikiliavyo. Wewe ni mama chukua jukumu la kulea mtoto au watoto wako asije(wasijekukuliza) akakuuliza pindi mtakapokuna mbinguni kwa Baba halafu ukashindwa la kujibu. Nakupenda mama yangu na nipo salama siku zote, sina hofu kwa kuwa unalinda na kunitetea siku zote!! Nani kama Mama Maria?       
  Naomba tumuige mama Maria kwa kazi nzuri anayoifanya kutulea sisi watoto wake.  Mama maria ni mama wa Yesu lakini ni mama yetu pia na ni msimamizi mkuu wa wazazi wetu. Mwenye heri Joseph Allamno mwanzilishi wa shirika letu la Consolata, alimkabizi shirika hili kwa Bikira Maria Consolata (Consolata maana yake mfariji), akiamini ya kuwa mama hamtupi mwanaye hata akiwa msumbufu kwa kiasi gani. Mama Maria ambaye ni msimamizi wa shirika letu la Consolata, hajatuache, yupo pamoja nasi kila siku akituongoza na kutuombea kwa mwanae mpendwa. Tunapozungumzia mafanikio tunatambua ya kuwa, Mama Maria yupo nasi. Mama Maria yupo nasi katika shida zetu, magumu, matatizo na katika changamoto zote zinazotupata bado anatuongoza, neema na faraja tuzipatazo ni kazi ya Mama yetu Maria.  
  Tujifunze mambo yafuatayo kutoka kwa Mama yetu Maria; kuwa tayari kuitikia wito wa Mungu, tuwe tayari kusema, nipo tayari kwa kazi ya Mungu, tuwe watu wasala, wanyenyekevu, wasikivu na wavumililivu. Tuitikia wito kama Mama yetu Maria bila kusita wala woga wowote kwani Mungu hatuachi pekee yetu katika magumu ya namna yoyote na shida zetu za kila siku.  Ukisema upo tayari anakuombea siku zote na Mungu atakuongoza katika wito wako wowote ule. Tukumbuke maneno mazuri ya Mama Maria alipotokewa na Malaika Gabriel alisema, “tazama, mimi ni mjakazi wa Bwana; na iwe kwangu kama ulivyosema.” (Rejea Luka 1:38).      
   Silaha ya uvulimilivu. Wengi wetu hatuna uvumilivu ni wepesi wa kukata tamaa hasa pale tunapopatwa na magumu katika maisha yetu. Katika ugonjwa, mateso na manyanyaso, katika masomo yetu, katika malezi yetu na mengine mengi. Tumwombe Mama Maria atupatia neema na nguvu za kuvumila mateso yetu. “Na penye msalaba wake Yesu walikuwa wamesimama mamaye, na umbu la mamaye, Mariamu wa klopa, na Mariamu Magdelene.” (Rejea Yohane 19:25-26). Hapa inatuonesha kuwa Mama Maria alivumilia sana kuona mateso ya mwanaye na bado hakumuacha. Je wewe ungefanyaje? Kwa nini unamkataa au kumkuna mwanao awapo katika mateso? 
   Mama Maria anatuonesha moyo wa unyenyekevu. Inatupasa kuwa wanyenyekevua katika maisha yetu tukitambua fadhila mbalimbali tunazotendewa na wenzetu. Mungu anatutaka tuwe wanyenyekevu hasa kwa karama mbalimbali anazotupatia. “Moyo wangu wamwadhimisha Bwana, na roho yangu imefurahia Mungu, mwokozi wangu; kwa kuwa ameutazama unyonge wa mjakazi wangu…”(Rejea Luka 1:46-55). Haya maneno yalitamkwa na Mama Maria, alijinyenyekeza kwa makuu ambayo Mungu alikusudia kumtendea.”Siku zote hatuwezi kuelewa pasipo kusijilizana, je unamsikiliza mwenzako aongeapo au kila mtu anaongea wala hakuna wa kumsiliza wenzake? 
   Mama Maria leo anatutaka kusikilizana. Lazima awepo muongeaji na msikilizaji pia hapo tuwaweza kuelewa. Hebu firia, Mama Maria asingemsikiliza Malaika Gabriel kungetokea kitu gani? Tumeona kuwa Mama Maria alimsikiliza na akapokea ujumbe wa Mungu. Na ndio maana aliweza hata kuuliza maswali ili aweze kuelewa zaidi. “Salamu hii ni ya namna gani?” (Rejea Luka 1:29); “Litakuwaje neno hili, maana sijui mume?” (Rejea Luka 1:34).  
   Nawatakieni kila laheri na Baraka tele katika maisha yenu, ila tutambue kuwa Mama Maria ni kimbilio letu, yupo siku zote akitulilia hasa tutendapo mabaya. Tumwombe yeye atatusaidia kwani ni mwombezi wetu mkuu, anatuombea kwa mwanaye pia kwa Baba yetu wa Mbinguni. Mama ninakupenda sana, umeteseka wa ajili yangu, umekimbiwa na baba kwa ajili yangu, na bado unaendelea kunihangaikia siku zote bila kukata tama, jipe moyo, Mama Maria yupo nawe siku zote. 
   Neema ya Bwana wetu Yesu Kristu ikae nasi, kutuongoza katika maisha yetu, hasa kwa kutambua umuhimu wa wazazi wetu, tuwaombee bila kuchoka, kwani hii ndio fadhila yetu kuu. Pia atusaidie kutimiza wajibu wetu na kutambua wito wetu katika dunia hii. Mungu atubariki sote!!!      

                                                
                   Na,    Frt. Benedict T. Msigwa, Morogoro.





KIFO CHA PADRE MASSAWE LELLO 



HABARI KUTOKA TANZANIA Oktoba 26, 2012: Rev Fr. Salutaris Massawe, IMC 
CHANZO CHA   HABARI: IMC TANZANIA  
Ndugu washirika na Watu wa Mungu, jana Oktoba 25, 2012   wakuu wote wa IMC bara (Africa)  walikwenda kwa ajili ya outing. Kwa bahati mbaya, Fr. Lelo Massawe Salutaris, Mkuu wa shirika kwa  Tanzania alipotea.  Alikuwa kuzama. Asubuhi hii, Oktoba 26, 2012 wameukuta mwili. Naomba Bwana kumpa mapumziko ya milele. Kwa familia yake ya  nasi  IMC  kwa Tanzania, tunfikisha rambirambi zetu na kuomba Mungu kwa aeendelee kuwaangalia. Mungu awabariki! 
Fr. Jean-Marie BILWALA, IMC

Dio è così grande e Quello che vuole lo compie!!!! anche se a volte non è facile comprendere!!!! Padre Lello resta in pace, Prega per noi che siamo ancora in Cammino
. Eterno riposo dona lui signore...,
Tunasikitika Kuondokewa na mkuu wa shirika letu Tanzania ila ni mipango ya Mungu anavuna atakako, Padre Lello Utuombee tufuate na kutunza ulicheanzisha!!!! Laha ya milele umpe ee Bwana na Mwanga wa milele Umwangazie, Apumzike kwa amani..
Danstan Mushobolozi - Italy
 I am very sorry to you all. we needed him but God needed him the most. the Lord gave the Lord has taken ........... the name of the Lord be in our minds all the times..........!!!!
Camilo Mlowe - Morogoro, Tanzania.


tulikupenda sana baba yetu Massawe, utumishi wako uliotukuka, ucheshi na uchangamfu wako, zaidi ulipenda kutupa moyo. basi Mungu kakupenda zaidi, tuombea nasi huko mbinguni kwenye makazi yetu ya milele.

Benedict Thomas - Morogoro, Tanzania

Hili ni pigo kwa region ya Tanzania, mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi Amina. 

 raha ya milele umpe ebwana na mwanga wa milele umwangazie astarehe kwa amani amina
Mathew Gaithan - Morogoro Tanzania









MAISHA HAYA YA FISI MPAKA LINI?
Na,  Frt. Benedict Thomas, Allamano 

  Nilipokuwa mtoto mdogo mara nyingi bibi yangu alikuwa akinisimulia hadithi nyingi zilizokuwa zinamhusu mnyama fisi. Nilikuja kukugundua mara zote katika hadithi hizo utasikia fisi akiambatana na mnyama sungura kama rafiki yake mkuu. Fisi kutokana na tabia yake alijikuta mara nyingi akiingie mkenge, mara kakamatwa na kuadhibiwa na binadamu au wanyama wengine. Lakini sungura wakati wote alijikuta hayupo katika mitego hiyo kwa sababu tu ya ujanja wake.
            Kwa kifupi fisi hakuwa na uamzi wa kuchagua, kila kitu alikuwa akitaka haijalishi uzuri wake au ubaya wake kila kitu alikitamani, na zaidi ya hayo alikuwa akidanyanyika kwa vitu visivyo halisi. Akialikwa katika sherehe mbili ambazo zote zinafanyika siku na wakati mmoja zote alitaka kuhudhuria na kujikuta hafaidi chochote na kuishi kukosa. Kwa ujumla maisha ya fisi yamejaa tamaa, hulka na ubinafsi na hana muda wa kuchambua kwani anachoangalia ni maslahi yake na si vingenezo. Ukimtadhimini mnyama fisi utagundua kuwa ni mwoga, hana ujasiri, chakula chake ni mabaki tu (mizoga).
            Sasa jiulize tokea lini wewe umekuwa fisi? Kila kitu unataka wewe upate, tena hata huangalii njia sitahiki ya kufikia hicho unachokitamani.  Maisha haya ya ufisi yanajionyesha katika mazingira mbalimbali kama rushwa, uroho wa madaraka, wivu, utoaji mimba, dhuruma na mambo mengine mengi.
            Mtaalamu mmoja wa falsafa Thomas Hobbes aliwahi kusema kuwa binadamu kwa asili yake ni mbinafsi, nadhani hilo huwezi kulipinga, na kama huamini chunguza maisha yako. Ni kweli binadamu lazima ahangaike katika kutafuta ridhiki yake, lakini mara nyingi amejikuta akiishi maisha ya ufisi, yaani yaliyojaa tamaa na ni mtu asiyeridhika hata kwa kikubwa alichonacho. Kama unabisha waliuliza matajiri wa dunia hii kama wamewahi kuridhika na walivyonavyo, sembuse wewe?













Uhai ni zawadi ya pekee kutoka kwa Mungu. Wototo ni majaliwa ya Mungu. Kwahiyo ni wazi kuwa, watoto ni zawadi ya pekee kutoka kwa Mungu. Tunaona ni jinsi gani watu wanavyotafuta watoto, katika mazingira ambayo tumekutana nao, na hata hivyo katika biblia tunasoma na kuthibitisha ukweli huu. Tunaona Sarai mkewe Abrahamu alikosa mtoto na alikuja kupata  badaye mtoto wa pekee  Isaka.  Tunamuona Rahel na hadithi yake inafanana na hiyo, na wengine wengi. Si hao tu katika biblia, bali hii ni hali  halisi pia katika mazingira tunamoishi. Lakini chakushangaza tunaona wengi wanapingana na zawadi hii (bila huruma), tukianza na herode, alivyo jaribu kumuangamiza Yesu, na baadaye akawauwa watoto wengine wengi. pia. Katika jamii ya sasa kuna wale wanao watelekeza watoto wao,  pia wanaowatupa majalalani watoto wao nk.
Kuna tafsiri mbalimbali mbali juu ya mtoto ni nani? Lakini, leo tutashirikiana kuwatazama, binadamu waadilifu wasiozidi miaka kumi. Ninamaanisha tupo huru kuwazungumzia wale wenye miaka sufuri hadi hicho kikomo nilichotaja.


X
 Nimevutiwa kuandika kifungu hiki kwa sababu ya  hazina kubwa iliyo ndani ya watoto wetu. Pia malezi wanayopata watoto yanamchango mkubwa katika kuandaa watu wa baadaye (hasa kisaikologia na Nyanja zinginezo). Waswahili husema “Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo.” Kumbe basi, tukiwalea watoto hawa katika mazingira ya maadili mema, ndivyo watu wa kisho watakavyo kuwa waadilifu; watakuwa wema na msaada katika jamii yote kwa ujumla. Lakini wakilelewa katika mazingira ya kikatili, kifisadi, kiwazi, n.k., ndivyo    watakavyo jiimarisha kwa tabia hizo yaani, makatili, mafisadi, wezi, kujumulisha sugu.  Na hii haipingiki kuwa ni hasara kwa wazazi na jamii kwa ujumla.

Tofauti katika uwezo mbalimbali kijinsia
Tofauti hizi ni kutokana na wataalamu mbalimbali waliofanikiwa kuchunguza tabia mbalimbali juu ya jinsia mbili na kwa wakati huu hasa kwa watoto wadogo ambao baadaye, kwa matumaini watakuwa watu wa umri wa utu uzima. Na hatimaye tofauti hizi hazi lengi katika kuwagombanisha au kutafuta nani anafaa zaidi, bali ni katika kusaidia kuleana na kuboresha ubinadamu wetu, kwa kadiri ya makusudi ya mungu.
Kuona, watoto wakike wanauwezo wakuona zaidi karibu kuliko wa kiume. Ndio maana takwimu zinaonesha kuwa, ajali za barabarani hasa zinazowahusu watoto wadogo; idadi ya watoto wa kiume ni zaidi ya wale wa kike.Hivyo, wazazi, walezi na jamii yote kwa ujumla ni vema wakafahamu hilo kisha waelekeza maarifa yao katika kuwasaidia kwa kadiri ya mahitaji.
Kusikia, inasemekana kuwa watoto wakike ni wapesi kusikia kuliko wa kiume. Ndio maana husemwa kuwa, mtoto wakike kwa umri wa wiki moja anaweza kutofautisha sauti ya mama yake na sauti za watoto wengine wakilia. Kitu ambacho ni mtihani kwa mtoto wa kiume.
Kuongea, watoto wakike wanakuza uwezo wakuongea zaidi kuliko wa kiume. Ndio maana husemwa kuwa, jinsia ya kiume inahitaji wastani wa maneno 700 ya kuwasiliana kwa siku wakati jinsia ya kike wanahitaji wastani wa maneno 20,000 kwa siku.
Kuwanyamazisha, tofauti hii inaendana na hiyo hapo juu. Watoto wakike wakilia hunyamazishwa kwa kukuimbiwa ikikululu. Wakati watoto wa kiume, hunyamazishwa kwa kuwaongelesha au kwa michezo mbalimbali. Kuna hadithi iliyo mshusha nyoka mtini akitamani kumsahihisha binadamu iliyekosea katika ugawaji. (huyu binadamu alimpa mbwa wake nyasi na mbuzi wake nyama na mifupa. Wakati huohuo akiwa amewafunga kamba mbali mbali ili wasiingiliane katika mgawanyo huo). Bilashaka hata wewe ungetelemka mtini ili usahihishe mgawanyo huo.  Hivyo tuwasadie bila kukosea nani ni nani na anahitaji nini katika mda na wakati ufaao.
 Pia, watoto wa kike wanapenda watu zaidi wakati wale wakiume wanapenda vitu.  Ndio maana watoto wa kike huzichukulia fimwanansensere (toys) kama marafiki. Na hivyo watoto wakike huweza kutazama na kutofautisha sura za watu wa familia na wageni katika umri wa wiki kumi na mbili wakati jambo hili ni kitendawili kwa watoto wa kiume.

Maendeleo ya ki-akili
Kama ilivyo kukua pia maendeleo ya akili hukua hatua kwa hatua. Hebu tazama pia majibu wanayotoa kwa maswali mbalimbali kwa watoto wanaoweza kuongea au kujieleza. Familia inapatikana wapi? wengine husema nyumbani, wengine  husema mbinguni, wengine husema kanisani, haya yote ni majibu sahihi hasa kwao kutokana na malezi na mazingira yanayo wazunguka. Swali jingine familia ina watu gani? Wengine husema (baba na mama), wengine husema (bibi na babu), wengine ni (mjomba na wifi), wengine walisema ni (baba, mama, kaka, dada na mtoto). Chakufurahisha ni kuwa majibu ya watoto hawa hayako mbali sana na uhalisia. Yaani yanategemea sana mafundisho wanayopata na mazingira wanayoishi. Hivyo si ajabu katika swali “Kazi ya baba ni nini?” kupata majibu yafuatayo: kunywa pombe (kulewa), wengine kuleta mahitaji, kulima, kwanda kazini, na wengine, kugombeza familia, kuadhibu watoto vikali wanapokosea, kuchelewa kuja nyumbani. Majibu haya yote yanawaza kuwa si sahihi katika mitihani ya darasani,
 lakini yana usahihi wake katika halihalisi ya maisha kwa kuwa yanaakisi na kusadifu mazingira halisia. Pia kondoo ni nini? Ni mbuzi?  linaweza kuwa ni jibu kwa swali hili.
                 Ndugu msomaji waswahili husema “Mkuki kwa nguruwe kwa binadamu…?” ni rahisi kuuliza na kupata majibu. Hapa ndipo kipima joto kilibadili uelekeo. Kama umezoea kuuliza basi tuone wewe unajibuje? Mimi niliuzwa swali na mdogo   wangu, ndio nikasikilizia joto lake!! Swali liliulizwa kwa heshima kabisa, kwamba kaka “Je vifaranga vikifa vinaenda mbinguni…..?”
Kuhusu mawazo mengine watoto wanamitazamo ifuatayo. Kuhusu maisha (life), kwao kila chenye mwendo kina uhai, hivyo hata gari lina uhai. Kuhusu kifo wengine wanafikiri kuwa si kitu cha kudumu. Hivyo wanaweza kuuliza, kwa nini waliokufa hawarudi? Uzito kwao ni sawa na ujazo, mfano debe moja la manyoya kwao lina uzito sawa na debe moja la mahindi. Wanaweza kuelewa namba 1-5, zaidi ya hapo, wanahesabu tu bila kuelewa. Kuhusu muda hawawezi kutofautisha usiku na mchana. Hawawezi kutofautisha wiki, siku saa nk. Mfano sentensi “Nilikuja kesho na nitakuja jana” zinaweza kuwa sahihi kwao.  Kwa sababu ya uhaba wa nafasi naomba kwa leo niishie hapa. Ni ushauri wangu kuwa tuwapende watoto wetu, tuwatunze watoto wetu, na tuwalee vizuri watoto wetu. maana ni tumaini la kanisa na pia ni taifa la kesho, bila kusahau mchango wao leo. Mungu na atubariki na kutuangazia uso wake.



No comments:

Post a Comment