ALLAMANO SEMINARI
Ni seminari ya shirika la
wamisionari wa Consolata ambao wanafanya kazi katika nchi mbalimbali zaidi ya
ishirini. Na hapa Tanzania wapo katika majimbo ya Dar-es-saalam, Iringa,
Njombe, Morogoro, Singida, na sasa wameanza utume katika jimbo la Dodoma.
Seminari hii ilianzishwa mwaka
1993, na mpaka sasa imetoa mapadre ambao wanafanya kazi katika nchi mbalimbali
na waseminari ambao wanaendelea na masomo yao katika nchi mbalimbali wakiwa
katika hatua mbalimbali. Hii ni nyumba ya malezi ambapo vijana wenye nia ya
kujiunga na shirika wanapata malezi pamoja na kusoma masomo ya Falsafa ambapo
kijana anasoma kwa kiwango cha Shahada.
Seminari hupokea vijana kutoka
mikoa mbalimbali hapa nchi ambao hujiunga baada ya kumaliza kidato cha sita na
kuwa na sifa za kuendelea na chuo kikuu. Kabla ya kuingia katika nyumba hii ya
malezi, kijana hutakiwa kuwa na mawasiliano na mkurugenzi wa miito wa shirika
kwa kuandika barua ya maombi na ikiwezekana kuonana naye.