Baada ya kuogelea kwa muda, ndipo Mapadre hao
walipoamua kutoka majini ili kurudi nyumbani, ghafla Padre kutoka Kongo
alishangaa kutomuona mwenzake, aliamua kurudi nyuma ili kumuangalia, ndipo
alipotoka majini na kutoa tarifa kwa wenzake kuhusu kutoonekana kwa Padre
mwenzao (Padre Masawe). Baada ya kumtafuta bila mafanikio siku iliyofuata
walimkuta amefariki akiwa ufukweni mwa baharí.
Tarifa za kifo cha Padre Masawe (Mkuu wa
shirika la Consolata Tanzania) zilianza kuenea baada ya kuthibitika kwa kifo
chake, watu mbalimbali walianza kutuma salamu za rambirambi kwa ndugu Wa
Consolata popote walipo. Mimi binafsi niliposikia
habari za kifo cha Padre Masawe, niliumia sana, nilipatwa na maumivu makali
sana ndani ya moyo wangu, furaha yote ya sikukuu ya iddi iliniisha. Ingawa Padre
Masawe sikuwahi kumuona kwa sura enzi ya uhai wake.
Kwanini
Niliumia Kutokana na KIFO Chake?????????
MCONSOLATA, naamini kwamba miongoni mwa watu waliokuwa wanatuombea wanafunzi wa shule ya Seminary ya Consolata, Padre Masawe naye alikuwa miongoni mwao, hivyo maombezi yake kwa Mama Bikira Maria Consolata (Mfariji) yalinifanya nisome vizuri, niwe na afya njema, na vilevile ni faulu vizuri masomo yangu.
Pili; Niliumia kwa sababu tangu nilipoanza kumsikia
Padre Massawe hata kabla ya kuwa Mkuu wa shirika hapa Tanzania, kwanza nilisikia
utendaji wake wa kazi ambapo kila kazi aliyopewa na shirika aliifanya kwa
weledi na majitoleo makubwa. Hivyo shirika limepoteza tunu kubwa sana.
Tatu; Mawazo
yake ya kimapinduzi katika Shirika la wa CONSOLATA yamepotea ghafla.
Nne;
Wamisionari wa Consolata sio kwa upande wa Tanzania tu, bali na Dunia kwa
ujumla wamepoteza kijana shapu, shupavu na mchapakazi.
Tano;
Wamisionari wa Consolata wanajishughulisha na kazi mbalimbali za kijamii, JUA
lililozimika ghafla (Padre Masawe), alikuwa na vipindi katika redio Tumaini na
alisimamia gazeti la “ENENDENI” la wamisionari wa Consolata Tanzania, hivyo
basi, mawazo yake ya kimapinduzi katika jamii ya Tanzania hatutayapata tena.
Sababu hizo za msingi ndizo zinazoniumiza sana moyoni mwangu.
Poleni sana Ndugu zangu wapendwa wa Consolata
kwani JUA lililozimika ghafla lilikuwa na
mawazo ya kimapinduzi, Mpenda Elimu na Muombezi wetu sisi wa Consolata (Mimi
sio Mseminari wa Shirika la Consolata, ila ni MCONSOLATA kwa sababu elimu yangu
na malezi mazuri nimeyapata seminari ya Consolata – Mafinga Iringa), pia JUA
hilo lilikuwa ni muombezi wa Kanisa la Mungu na Dunia kwa ujumla.
“JUA” lililozimika uzidi kutuombea sisi
uliotuacha katika dunia hii na sisi pia tunazidi kukuombea ili upumzike kwa
Amani.
BWANI ALITOA
BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIHIMIDIWE AMINA.
Mama ni mlezi mkuu wa familia. Ni
mama ambaye anahusika katika kulea watoto wake pamoja na mumewe kama anaye. Tunamhitaji
mama katika maisha yetu. Ni nani asiyetambua umuhimu na upendo wa mama? Achilia
mbali kwamba kuna siku aliwahi kukuumiza ukafikia hatua ya kusema huyu si mama
yangu. Au alifanya jambo ambalo mpaka sasa ukifiria halikuingia akili mwako, na
kama ni kweli mama yako alifanya hivyo, lakini tambua mama ni mama na atabaki
kuwa mama yako. Anaudhaifu na mapungufu yake kama binadamu lakini bado
anayonguvu ya kusema mwangu, umenisumbua sana katika utoto wako, ujana na hata
katika uzee wako bado sikukuache. Tunamtambu mama kwa majukumu mengi aliyanayo
hususani mama ni mlezi mkuu wa familia.
Mama huyu anakutana na magumu mengi
lakini bado hakati tamaa, anajijengea moyo wa uvumilivu hata kama mateso
anayoyapata yanakatisha tamaa, lakini anajipa moyo akiamini ipo siku
yatakwisha. Inanisikitisha sana kuna baadhi ya akina mama au dada hawapo tayari
kupokea majumu ya kulea familia, utasikia wakisema ili kuwa bahati mbaya,
sikudhamiria kulea, mimi bado mwanafunzi, haukuwa mpango wangu, alinidanganya
nikaamua kufanya hivyo. Tambueni kwa Mungu hakuna bahati mbaya, yote yanapangwa
kutendeka wakati utimiapo, kwani hafikiria vile binadamu afikiliavyo. Wewe ni
mama chukua jukumu la kulea mtoto au watoto wako asije(wasijekukuliza) akakuuliza
pindi mtakapokuna mbinguni kwa Baba halafu ukashindwa la kujibu. Nakupenda mama
yangu na nipo salama siku zote, sina hofu kwa kuwa unalinda na kunitetea siku
zote!! Nani kama Mama Maria?
Naomba tumuige
mama Maria kwa kazi nzuri anayoifanya kutulea sisi watoto wake. Mama maria ni mama wa Yesu lakini ni mama yetu
pia na ni msimamizi mkuu wa wazazi wetu. Mwenye heri Joseph Allamno mwanzilishi
wa shirika letu la Consolata, alimkabizi shirika hili kwa Bikira Maria Consolata
(Consolata maana yake mfariji), akiamini ya kuwa mama hamtupi mwanaye hata
akiwa msumbufu kwa kiasi gani. Mama Maria ambaye ni msimamizi wa shirika letu
la Consolata, hajatuache, yupo pamoja nasi kila siku akituongoza na kutuombea
kwa mwanae mpendwa. Tunapozungumzia mafanikio tunatambua ya kuwa, Mama Maria
yupo nasi. Mama Maria yupo nasi katika shida zetu, magumu, matatizo na katika changamoto
zote zinazotupata bado anatuongoza, neema na faraja tuzipatazo ni kazi ya Mama
yetu Maria.
Tujifunze mambo yafuatayo kutoka kwa
Mama yetu Maria; kuwa tayari kuitikia wito wa Mungu, tuwe tayari kusema, nipo
tayari kwa kazi ya Mungu, tuwe watu wasala, wanyenyekevu, wasikivu na wavumililivu. Tuitikia wito kama Mama yetu Maria
bila kusita wala woga wowote kwani Mungu hatuachi pekee yetu katika magumu ya
namna yoyote na shida zetu za kila siku.
Ukisema upo tayari anakuombea siku zote na Mungu atakuongoza katika wito
wako wowote ule. Tukumbuke maneno mazuri ya Mama Maria alipotokewa na Malaika
Gabriel alisema, “tazama, mimi ni mjakazi wa Bwana; na iwe kwangu kama
ulivyosema.” (Rejea Luka 1:38).
Silaha ya uvulimilivu. Wengi wetu
hatuna uvumilivu ni wepesi wa kukata tamaa hasa pale tunapopatwa na magumu
katika maisha yetu. Katika ugonjwa, mateso na manyanyaso, katika masomo yetu,
katika malezi yetu na mengine mengi. Tumwombe Mama Maria atupatia neema na nguvu
za kuvumila mateso yetu. “Na penye msalaba wake Yesu walikuwa wamesimama mamaye,
na umbu la mamaye, Mariamu wa klopa, na Mariamu Magdelene.” (Rejea Yohane 19:25-26).
Hapa inatuonesha kuwa Mama Maria alivumilia sana kuona mateso ya mwanaye na bado
hakumuacha. Je wewe ungefanyaje? Kwa nini unamkataa au kumkuna mwanao awapo
katika mateso?
Mama Maria anatuonesha moyo wa
unyenyekevu. Inatupasa kuwa wanyenyekevua katika maisha yetu tukitambua fadhila
mbalimbali tunazotendewa na wenzetu. Mungu anatutaka tuwe wanyenyekevu hasa kwa
karama mbalimbali anazotupatia. “Moyo wangu wamwadhimisha Bwana, na roho yangu
imefurahia Mungu, mwokozi wangu; kwa kuwa ameutazama unyonge wa mjakazi
wangu…”(Rejea Luka 1:46-55). Haya maneno yalitamkwa na Mama Maria,
alijinyenyekeza kwa makuu ambayo Mungu alikusudia kumtendea.”Siku zote hatuwezi kuelewa pasipo
kusijilizana, je unamsikiliza mwenzako aongeapo au kila mtu anaongea wala hakuna
wa kumsiliza wenzake?
Mama Maria leo anatutaka kusikilizana. Lazima awepo
muongeaji na msikilizaji pia hapo tuwaweza kuelewa. Hebu firia, Mama Maria
asingemsikiliza Malaika Gabriel kungetokea kitu gani? Tumeona kuwa Mama Maria
alimsikiliza na akapokea ujumbe wa Mungu. Na ndio maana aliweza hata kuuliza
maswali ili aweze kuelewa zaidi. “Salamu hii ni ya namna gani?” (Rejea Luka
1:29); “Litakuwaje neno hili, maana sijui mume?” (Rejea Luka 1:34).
Nawatakieni kila laheri na Baraka
tele katika maisha yenu, ila tutambue kuwa Mama Maria ni kimbilio letu, yupo
siku zote akitulilia hasa tutendapo mabaya. Tumwombe yeye atatusaidia kwani ni
mwombezi wetu mkuu, anatuombea kwa mwanaye pia kwa Baba yetu wa Mbinguni. Mama
ninakupenda sana, umeteseka wa ajili yangu, umekimbiwa na baba kwa ajili yangu,
na bado unaendelea kunihangaikia siku zote bila kukata tama, jipe moyo, Mama
Maria yupo nawe siku zote.
Neema ya Bwana wetu Yesu Kristu ikae
nasi, kutuongoza katika maisha yetu, hasa kwa kutambua umuhimu wa wazazi wetu,
tuwaombee bila kuchoka, kwani hii ndio fadhila yetu kuu. Pia atusaidie kutimiza wajibu wetu na kutambua wito wetu katika dunia hii. Mungu atubariki sote!!!
KIFO CHA PADRE MASSAWE LELLO
HABARI KUTOKA TANZANIA Oktoba 26, 2012: Rev Fr. Salutaris Massawe, IMC
CHANZO CHA HABARI: IMC TANZANIA
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgmCpKjyKEf_bA11V0Qs0iuxygByJ6hkyOigCXc2OTVTdr0sVD8lFX3hAqNgdZ9-EAs0PIlyaBj33IPequ83k24FA0TMz3CaWitGE8te38T8C-dPuwiXY79s6TZXhDK2_m2jTWf0kJgIcr5/s200/MPYA.jpg)
Fr. Jean-Marie BILWALA, IMC
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgFwvV0czkO36SwvAdLy6ALuuP17GbC36lc84UKugJigdo9D08g8lj5rG0315x0vPWBNPzq87CGinWiyTUNtgRUUIP764e6efFsgKXLsNRIh8PHEqXfD7lSziUhJWacAE3LN4phU8n5nSWB/s400/MP.jpg)
Dio è così grande e Quello che vuole lo compie!!!! anche se a volte non è facile comprendere!!!! Padre Lello resta in pace, Prega per noi che siamo ancora in Cammino
. Eterno riposo dona lui signore...,Tunasikitika Kuondokewa na mkuu wa shirika letu Tanzania ila ni mipango ya Mungu anavuna atakako, Padre Lello Utuombee tufuate na kutunza ulicheanzisha!!!! Laha ya milele umpe ee Bwana na Mwanga wa milele Umwangazie, Apumzike kwa amani..
Danstan Mushobolozi - Italy
I am very sorry to you all. we needed him but God needed him the most. the Lord gave the Lord has taken ........... the name of the Lord be in our minds all the times..........!!!!
Camilo Mlowe - Morogoro, Tanzania.
tulikupenda sana baba yetu Massawe, utumishi wako uliotukuka, ucheshi na uchangamfu wako, zaidi ulipenda kutupa moyo. basi Mungu kakupenda zaidi, tuombea nasi huko mbinguni kwenye makazi yetu ya milele.
tulikupenda sana baba yetu Massawe, utumishi wako uliotukuka, ucheshi na uchangamfu wako, zaidi ulipenda kutupa moyo. basi Mungu kakupenda zaidi, tuombea nasi huko mbinguni kwenye makazi yetu ya milele.
Benedict Thomas - Morogoro, Tanzania
Hili ni pigo kwa region ya Tanzania, mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi Amina.
raha ya milele umpe ebwana na mwanga wa milele umwangazie astarehe kwa amani amina
Mathew Gaithan - Morogoro Tanzania
MAISHA HAYA YA FISI MPAKA LINI?
Na, Frt. Benedict Thomas, Allamano
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiyYYN053UJZzCF0tdA1Olnqk5GwEq5nT855bAG4o_rEy2ItK2VLhog8n2no84A2k-57kTwYM7qD6jpp6ku4UEOsHjhpU0vgUwahHcF2aaLLbZjWBjVli6XIuOPKaRg5GokIuQ53kOiPGQ/s320/hyena_knp-a7901g.jpg)
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjXwehdivQ2L1IKaGdPSZ95HJuExrZFnSCed4yBPnNYa0lwmaW44rpPrOYhyfkxhC4646M2jL_pTm7KnRqVCFbjdJEBxwbchWBAQI0b03k6SIXzzRp-wbnv4wXQu0twCllWsTVj9vwyaMg/s400/is.jpg)
Sasa jiulize
tokea lini wewe umekuwa fisi? Kila kitu unataka wewe upate, tena hata huangalii
njia sitahiki ya kufikia hicho unachokitamani.
Maisha haya ya ufisi yanajionyesha katika mazingira mbalimbali kama
rushwa, uroho wa madaraka, wivu, utoaji mimba, dhuruma na mambo mengine mengi.
Mtaalamu
mmoja wa falsafa Thomas Hobbes aliwahi kusema kuwa binadamu kwa asili yake ni
mbinafsi, nadhani hilo huwezi kulipinga, na kama huamini chunguza maisha yako.
Ni kweli binadamu lazima ahangaike katika kutafuta ridhiki yake, lakini mara
nyingi amejikuta akiishi maisha ya ufisi, yaani yaliyojaa tamaa na ni mtu
asiyeridhika hata kwa kikubwa alichonacho. Kama unabisha waliuliza matajiri wa
dunia hii kama wamewahi kuridhika na walivyonavyo, sembuse wewe?
Uhai ni zawadi ya pekee kutoka kwa Mungu. Wototo ni majaliwa ya Mungu. Kwahiyo ni wazi kuwa, watoto ni zawadi ya pekee kutoka kwa Mungu. Tunaona ni jinsi gani watu wanavyotafuta watoto, katika mazingira ambayo tumekutana nao, na hata hivyo katika biblia tunasoma na kuthibitisha ukweli huu. Tunaona Sarai mkewe Abrahamu alikosa mtoto na alikuja kupata badaye mtoto wa pekee Isaka. Tunamuona Rahel na hadithi yake inafanana na hiyo, na wengine wengi. Si hao tu katika biblia, bali hii ni hali halisi pia katika mazingira tunamoishi. Lakini chakushangaza tunaona wengi wanapingana na zawadi hii (bila huruma), tukianza na herode, alivyo jaribu kumuangamiza Yesu, na baadaye akawauwa watoto wengine wengi. pia. Katika jamii ya sasa kuna wale wanao watelekeza watoto wao, pia wanaowatupa majalalani watoto wao nk.
Kuna tafsiri mbalimbali mbali juu ya mtoto ni nani? Lakini, leo tutashirikiana kuwatazama, binadamu waadilifu wasiozidi miaka kumi. Ninamaanisha tupo huru kuwazungumzia wale wenye miaka sufuri hadi hicho kikomo nilichotaja.
X
Tofauti katika uwezo mbalimbali kijinsia
Tofauti hizi ni kutokana na wataalamu mbalimbali waliofanikiwa kuchunguza tabia mbalimbali juu ya jinsia mbili na kwa wakati huu hasa kwa watoto wadogo ambao baadaye, kwa matumaini watakuwa watu wa umri wa utu uzima. Na hatimaye tofauti hizi hazi lengi katika kuwagombanisha au kutafuta nani anafaa zaidi, bali ni katika kusaidia kuleana na kuboresha ubinadamu wetu, kwa kadiri ya makusudi ya mungu.
Kuona, watoto wakike wanauwezo wakuona zaidi karibu kuliko wa kiume. Ndio maana takwimu zinaonesha kuwa, ajali za barabarani hasa zinazowahusu watoto wadogo; idadi ya watoto wa kiume ni zaidi ya wale wa kike. Hivyo, wazazi, walezi na jamii yote kwa ujumla ni vema wakafahamu hilo kisha waelekeza maarifa yao katika kuwasaidia kwa kadiri ya mahitaji.
Kusikia, inasemekana kuwa watoto wakike ni wapesi kusikia kuliko wa kiume. Ndio maana husemwa kuwa, mtoto wakike kwa umri wa wiki moja anaweza kutofautisha sauti ya mama yake na sauti za watoto wengine wakilia. Kitu ambacho ni mtihani kwa mtoto wa kiume.
Kuongea, watoto wakike wanakuza uwezo wakuongea zaidi kuliko wa kiume. Ndio maana husemwa kuwa, jinsia ya kiume inahitaji wastani wa maneno 700 ya kuwasiliana kwa siku wakati jinsia ya kike wanahitaji wastani wa maneno 20,000 kwa siku.
Kuwanyamazisha, tofauti hii inaendana na hiyo hapo juu. Watoto wakike wakilia hunyamazishwa kwa kukuimbiwa ikikululu. Wakati watoto wa kiume, hunyamazishwa kwa kuwaongelesha au kwa michezo mbalimbali. Kuna hadithi iliyo mshusha nyoka mtini akitamani kumsahihisha binadamu iliyekosea katika ugawaji. (huyu binadamu alimpa mbwa wake nyasi na mbuzi wake nyama na mifupa. Wakati huohuo akiwa amewafunga kamba mbali mbali ili wasiingiliane katika mgawanyo huo). Bilashaka hata wewe ungetelemka mtini ili usahihishe mgawanyo huo. Hivyo tuwasadie bila kukosea nani ni nani na anahitaji nini katika mda na wakati ufaao.
Maendeleo ya ki-akili
Kama ilivyo kukua pia maendeleo ya akili hukua hatua kwa hatua. Hebu tazama pia majibu wanayotoa kwa maswali mbalimbali kwa watoto wanaoweza kuongea au kujieleza. Familia inapatikana wapi? wengine husema nyumbani, wengine husema mbinguni, wengine husema kanisani, haya yote ni majibu sahihi hasa kwao kutokana na malezi na mazingira yanayo wazunguka. Swali jingine familia ina watu gani? Wengine husema (baba na mama), wengine husema (bibi na babu), wengine ni (mjomba na wifi), wengine walisema ni (baba, mama, kaka, dada na mtoto). Chakufurahisha ni kuwa majibu ya watoto hawa hayako mbali sana na uhalisia. Yaani yanategemea sana mafundisho wanayopata na mazingira wanayoishi. Hivyo si ajabu katika swali “Kazi ya baba ni nini?” kupata majibu yafuatayo: kunywa pombe (kulewa), wengine kuleta mahitaji, kulima, kwanda kazini, na wengine, kugombeza familia, kuadhibu watoto vikali wanapokosea, kuchelewa kuja nyumbani. Majibu haya yote yanawaza kuwa si sahihi katika mitihani ya darasani,
Ndugu msomaji waswahili husema “Mkuki kwa nguruwe kwa binadamu…?” ni rahisi kuuliza na kupata majibu. Hapa ndipo kipima joto kilibadili uelekeo. Kama umezoea kuuliza basi tuone wewe unajibuje? Mimi niliuzwa swali na mdogo wangu, ndio nikasikilizia joto lake!! Swali liliulizwa kwa heshima kabisa, kwamba kaka “Je vifaranga vikifa vinaenda mbinguni…..?”
Kuhusu mawazo mengine watoto wanamitazamo ifuatayo. Kuhusu maisha (life), kwao kila chenye mwendo kina uhai, hivyo hata gari lina uhai. Kuhusu kifo wengine wanafikiri kuwa si kitu cha kudumu. Hivyo wanaweza kuuliza, kwa nini waliokufa hawarudi? Uzito kwao ni sawa na ujazo, mfano debe moja la manyoya kwao lina uzito sawa na debe moja la mahindi. Wanaweza kuelewa namba 1-5, zaidi ya hapo, wanahesabu tu bila kuelewa. Kuhusu muda hawawezi kutofautisha usiku na mchana. Hawawezi kutofautisha wiki, siku saa nk. Mfano sentensi “Nilikuja kesho na nitakuja jana” zinaweza kuwa sahihi kwao. Kwa sababu ya uhaba wa nafasi naomba kwa leo niishie hapa. Ni ushauri wangu kuwa tuwapende watoto wetu, tuwatunze watoto wetu, na tuwalee vizuri watoto wetu. maana ni tumaini la kanisa na pia ni taifa la kesho, bila kusahau mchango wao leo. Mungu na atubariki na kutuangazia uso wake.
No comments:
Post a Comment