Saturday, December 1, 2012
Saturday, November 3, 2012
MISA
YA KUMUOMBEA MKUU WA SHIRIKA LA WAMISIONARI WA CONSOLATA TANZANIA PADRE SALUTARIS
LELLO MASAWE ALIYEFARIKI KWA AJALI YA MAJI HUKO BAGAMOYO TAREHE 25 OKTOBA,
2012.
Padre
Saltaris Masawe alikuwa Padre wa Shirika la Consoalata mzaliwa wa hapa
Tanzania, alipata daraja la Upadre mwaka 1993, jimboni Moshi mkoani
Kilimanjaro. Na amefanya kazi katika nchi mbalimbali ambako wamissionari wa
Consolata wanafanya kazi. Amewahi kufanya kazi nchini Ethiopia, Italia na
baadae shirika lilimtuma hapa Tanzania
ili arudi kuwaimarisha ndugu zake. Mara kwa mara Padre Lello alipenda kusema
hivyo kwamba amerudi kuwahudumia ndugu zake watanzania.
Tarehe
25 Oktoba, 2012 Padre Salutaris akiwa na wakuu wa shirika kutoka nchi nyingine
za Afrika alikwenda Bagamoya pamoja na mambo mengine walienda kuogelea kama
sehemu ya mapumziko yao, na hapo ndipo mauti yalimkuta akiwa anaogelea
Baharini, mwili wake ulionekana siku iliyofuata yaani tarehe 26 Oktoba.
Hapa
kwetu katika nyumba ya malezi ya Mwenye Heri Padre Yosefu Allamano Morogoro,
jioni ya tarehe 26 tulifanya Misa jioni saa kumi na mbili kwaajili ya kumuombea
Baba yetu Massawe na misa hiyo
iliongozwa na Padre Hipolith Marandu IMC ambae pia ni mlezi na mwalimu wa
Tauhidi (Teolojia) hapa seminarini. Katika Misa hiyo padre Marandu alimuelezea
marehemu alivyo mfahamu tangu alipokuwa nae Kenya akiwa shule, baadaye nchini
Italia na sasa akiwa hapa Tanzania. Alisema alikuwa ni padre aliyeuishi upadre
wake na alilihudumia shirika na kanisa kwa moyo wote, alililetea shirika
heshima kila alipotumwa kufanya kazi na yeye mwenyewe aliheshimika ndani ya
Tanzania na nje ya Tanzania. Alikuwa kweli mmissionari mwafrika ambae
hakujificha kuonesha uafrika wake popote alipokuwa. Aliporudi hapa nyumabani
alipewa kazi ya Gazeti la Enendeni, kazi ambayo aliifanya kwa weledi mkubwa na
hata kuliinua gazeti kuwa na hadhi sana hapa Tanzania. Mwaka jana mapadre wa
shirika la Consolata hapa Tanzania waliona ni vema wamkabidhi madaraka ya
kuliongoza shirika, nae kwa moyo mkuu aliipokea hiyo kazi na akawa Padre
mwafrika mconsolata wa kwanza kuwa mkuu wa shirika hapa Tanzania. Padre Marandu
alitualika kusali kwaajili ya shirika hapa Tanzania na ulimwenguni kote, lakini
pia kwaajili ya familia yake, Mungu aendelee kuwa pamoja nao katika kipindi
hiki kugumu cha maomboleo.
Siku
iliyofuata tulisali misa maalumu ya kumuombea baba Masawe, siku hii tukiungana
na ndugu zetu kutoka nyumba ya malezi Pre-Philosophy Makunganya na dada zetu
masista wanaokaa katika nyumba ya malezi Mkundi. Misa iliongozwa na Padre Isaac
Nabea Mbuba imc (Mlezi Pre-Philosophy) akisaidiwa na Mapadre; Wiliamu Mkalula
imc, Hipolith Marandu imc, Jude Katende imc (Mlezi Pre-Philosophy). Baada ya
misa takatifu tulipata muda kidogo wa kutafakali namna tulivyomfahamu na tulivyoishi na Padre Masawe kabla ya kuondoka
hapa duniani.
Pd.
William Mkalula imc
Pamoja
na kuonesha namna alivyomfahamu Pd. Masawe, alienda mbali zaidi akisema sifa
muhimu ambazo zingetusaidia sisi kama walelewa; alimwelezea padre masawe kama
mtu aliyeupenda Upadre wake na umissionari wake. Yeye alimufahamu zaidi Pd.
Masawe kwasababu ya vile alivyokuwa anatimiza wajibu wake kwa umakini. Njia
pekee ya kumuenzi mkuu wetu wa shirika ni kuyatekeleza na kuyafiuata yale
ambayo mara zote alisisitiza hasa maisha ya jumuia na zaidi sana kuwa na nia
njema na shirika na kanisa. Tujitahidi kusonga mbele daima. Yeye mwenyewe
alisisitiza kwamba anamshuluru Mungu kwa sababau ni Mconsolata na anaupenda Uconsolata
wake. Jitahidini kuwa wakweli na wawazi kwa walezi wenu, alisema Pd. Mkalula. Wishoni
alimshuuru sana Pd. Isaac Mbuba kwa msaada wake katika maisha yake ya
kimisionari kwasababu kuna wakati amewahi kufanya nae kazi huko katika parokia
ya Heka.
Sr.
Thelesia Ponela imc
Sista ananza kwa kuelezea namna alivyofanya kazi na Pd.
Masawe kwa miaka miwili kule Bunju kituo cha mazoezi ya kiroho akiwa kama
Mkurugenzi wa Gazeti la ENENDENI hapa Tanzania. Anasema alikuwa ni Padre
mchapakazi na aliyejituma katika kazi zake. Alisisitiza muda wote maisha ya
familia, maisha ya kufanya kazi pamoja kwa umoja, hilo ndilo limebaki kwangu
kama kumbukumbu na anaendelea kunipa changamoto katika maisha yangu ya
umisionari, nijitahidi kupenda maisha ya jumuia. Sista anaongeza kwamba anafuarahi kuwa
Tanzania pamoja na matatizo yote. Matatizo yananifanya nisonge mbele kwa nguvu
na bidii. Tuutafute utakatifu kwa juhudi zote, tukijifunza utakatifu wa Baba
Allamano ambao haukuwa katika mambo makubwa naya ajabu bali mambo madogomadogo.
Tujitahidi twende kwa pamoja na kwa ujasiri mkuu.
Pd.
Mbuba Isaac imc
Padre alianza
kwa kuuuliza swali kwamba kwanini wazuri tu? Ninapotafakari msiba huu
ninakumbuka marehemu Padre Alexius Lipingu, Pd. Jachindo na waseminari wetu
waliotutoka wakiwa hapa Morogoro; Frt. Nchimbi na Frt. Jackson Chengula.
Tunamuomba Mungu awapokee na wawe waombezi wetu huko Mbinguni. Anatugeukia sisi
sote na kutuambia “Jipeni Moyo msiogope, songa mbele, (courage). Pd. Mbuba
anamshukuru Mungu kwaajili ya yote aliyofanya kwa njia ya mtumishi wake
Pd.Masawe, anasema Mkuu huyu wa shirika alianza kutukumbusha wajibu wetu kama
wamissionari na tusisinzie kamwe. Kwanini Mungu kamuchukua mapema hivi, wakati
shirika na kanisa likihitaji sana mchango wake?
Sr.
Elizabeth Msacky imc
Nikiwa bado
mdogo nilianza kujisikia wito, lakini sikuwa nafahamu chochote kuhusu mashirika
haya ya kitawa na wala sikuwafahamu waconsolata. Siku moja niliona kipeperushi
cha waconsolata na kwasababu Padre Masawe alikuwa anasoma pale Mwanza chuo
kikuu cha Mtakatifu Augustino na mara kwa mara nilikuwa namuona anongoza misa,
niliamua kumfuata kumuuliza waconsolata ni watu gani? Kwanza alinijibu kwamba
yeye ni Padre mconsolata na yupo pale kwa masomo, aliniahidi kunisaidia ili
niwe na wasiliano na mkurugenzi wa miito. Tangu hapo sikumfahamu mconsolata
mwingine ila Padre Masawe mpaka nilipokuja kuingia nyumba ya malezi. Akawa ni
msaada hata kwa familia yangu nyumbani, alimsaidia sana dada yangu katika ndoa
yake. Padre Masawe kweli alikuwa mfano wa kuigwa katika maisha yake ya utume,
Mungu amempenda zaidi kuliko sisi, basi tumuombee.
Sr.
Suzana Kiho imc
Padre Masawe
alisisitiza sana maisha ya pamoja katika yote, nasi tujifunze kwa mfano wake.
Alikuwa mtu wa kupokea watu, nasi tuwe watu kupokea wengine na kuwasaidia, na
ni lazima kujiuliza mara zote katika maisha yangu watu wanaonja nini kwangu?
Wanajifunza nini kwangu? Nikifa leo watu ninaowaacha waseme nini juu yangu?
Watu ni lazima wajifunze Upendo wa Mungu kutoka kwetu sote, waonje faraja
kwetu.
Frt.
Leonard Celestine Mihafu
Kifo kinapotokea
huleta changamoto kubwa kwetu hasa kwetu sisi vijana, na kwasababu kifo huzidi
hata Falsafa na Tauhidi (Teolojia) masomo tuyayasoma, basi tubaki na Imani kwa
Mungu. Lakini ni lazima tujue kuwa tuna kazi kubwa ya kuwa watakatifu na
kuwasaidia wengine wawe watakatifu kwa mifano yetu ya maisha ya kila siku. Lifo
cha Padre Masawe kibaki fundisho kwetu na tujiulize mimi je nikifa leo
itakuwaje? Wewe je ukifa leo?
Frt.
Patrick (Pre-Philosophy)
Ni wakati mgumu sana, na ni kipindi cha majozi mkubwa kwa
shirika na kwa kanisa nzima la Mungu. Lakini kwa hayo tunajifunza kuvumulia
magumu, tuchukue mazuri yote twende nayo na tuishi nayo ndio namna ya kumuenzi
Mkuu wetu wa shirika Padre Masawe.
Pd.
Hipolith Marandu imc
Nimekuwa naye
katika sehemu mbalimbali katika utume wake, nilikuwa nae Kenya wakati
nikifundisha pale, baadae tulikutana Italia katika utume wake. Alisema tunataka
akina Masawe wengine hapa seminarini. Tuwe watu wa maana na waungwana katika
umisionari wetu, tukiwajali watu wote kama njia ya kumpeleka Yesu aliye faraja
ya kweli kwa wote. Injili iwe taa ya kila mtu.
Monday, October 29, 2012
Saturday, October 27, 2012
BE READY
Friday, October 26, 2012
SAD NEWS
NEWS FROM TANZANIA OCTOBER 26, 2012: Rev. Fr. SALUTARIS MASSAWE, IMC
SOURCE OF INFORMATION: IMC TANZANIA REGION

Dear Confreres and People of God, yesterday October 25, 2012 all the IMC continental superiors went for outing. Unfortunately, Fr. Lelo Massawe Salutaris, the Regional Superior of Tanzania went missing. He was drown. This morning, October 26, 2012 they found the body. May the Lord give him Eternal Rest. For his family of origin and the entire IMC region of Tanzania, we convey our Condolences and pray God to keep on looking after them. God bless!
Sunday, October 21, 2012
Thursday, October 11, 2012
Subscribe to:
Posts (Atom)